Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawataarifu waombaji wote wa ajira waliotuma maombi kupitia mfumo wa e-Ajira Uhamiaji kutembelea akaunti zao kwenye https://www.immigration.go.tz na barua pepe zao kupata taarifa za tarehe na eneo la usaili kwa waliochaguliwa. Wasailiwa wanapaswa kuwa na Application ID, kitambulisho chenye picha, na kalamu ya wino wa bluu. Waombaji wa TEHAMA, udereva na ufundi magari wajiandae kwa usaili wa vitendo. Kila msailiwa atajigharamia chakula, usafiri na malazi. Kwa maswali: ajira@immigration.go.tz.