Tangazo Rasmi la Orodha ya Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Uhamiaji 2026 Kupitia Mfumo wa e-Ajira
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia vijana wote walioomba ajira kupitia Mfumo wa e-Ajira Uhamiaji kuwa majina ya waliochaguliwa kwa usaili yanapatikana kwenye akaunti zao za maombi. Waombaji wanapaswa kutembelea tovuti rasmi ya Uhamiaji https://www.immigration.go.tz pamoja na kukagua barua pepe walizotumia wakati wa kutuma maombi ili kupata taarifa kamili za tarehe, muda na eneo la usaili.
Wasailiwa wote wanatakiwa kufika wakiwa na Namba ya Ombi la Ajira (Application ID), kitambulisho halali chenye picha (kama NIDA, Kadi ya Mpiga Kura, Pasipoti au Kitambulisho cha Mkazi) pamoja na kalamu ya wino wa bluu. Waombaji wa fani za TEHAMA, udereva na ufundi magari wanapaswa kujiandaa kwa usaili wa vitendo (Practical Examination). Aidha, wasailiwa wote wanapaswa kujigharamia usafiri, chakula na malazi kwa kipindi chote cha usaili. Kwa mawasiliano au changamoto, wasiliana kupitia ajira@immigration.go.tz.